dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 15, 2017

ZANZIBAR: WAFANYABIASHARA WATAKA ZBS ITAMBULIKE TANZANIA!

SERIKALI imesema inatarajia kuweka mfumo maalumu wa kodi ili kuondosha vikwazo, kero, malalamiko na changamoto zinazojitokeza katika sekta ya biashara.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Kalid Salum Mohamed, alieleza hayo alipokua akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumalizika mazungumzo baina ya wafanyabiashara na wakala wa forodha yaliofanyika ukumbi wa wizara hiyo huko Vuga.

Alisema katika mwaka wa fedha 2017/2018, serikali imelenga kupitia upya mfumo wa kodi ili kuondosha kasoro na changamoto zilizopo.

Alisema dhamira ya kuwaita wafanyabiashara hao ni kutambua na kubaini vikwazo na malalamiko walionayo katika sekta ya biashara ikiwemo usafirishaji wa bidhaa.

Alisema mazungumzo hayo yatatoa fursa ya kuwasilisha changamoto zinazowakabilia wafanyabiashara katika kikao maalumu kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema serikali zote mbili zinaendelea kuweka mifumo bora ya kodi kwa ajili ya uimarishaji wa maendeleo yao pamoja na nchi.

Kuhusu baadhi ya malalamiko ya wafanyabiashara hao, alisema miongoni mwa kero na malalamiko yao tayari serikali zote mbili wameshayafanyia kazi likiwemo ulipaji wa VAT mara mbili Zanzibar na Tanzania Bara na kuondosha msongomano wa upatikanaji huduma za benki.

Kuhusu suala la ujenzi wa ‘Darajani Corridor’ alisema, lengo la serikali ni kuimarisha miundombinu ya kisasa ya kibiashara itakayotoa fursa za ajira, ukuzaji uchumi na kuwa kivutio cha wageni nchini.

Kuhusu ombi la wafanyabiashara juu ya kutambulika kwa taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Tanzania Bara kama inavyotambulika TBS, aliahidi kulifanyiwa kazi suala hilo huku akitoa ufafanuzi juu ya gari ziliosajiliwa Zanzibar kupatiwa kibali cha miezi mitatu.

Nae mfanyabiashara Ali Amour kwa niaba ya wafanyabiashara wenzakee alikiri kuwepo usimamizi na utekelezaji wa vitendo hususan kero za wafanyabiashara jambo ambalo litaleta ufanisi.

No comments :

Post a Comment