Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 29, 2017

Lissu amekaa mwenyewe kwa mara ya kwanza pasipo msaada!

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) leo amekaa mwenyewe pasipo msaada wa madaktari katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, anakotibiwa baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake, Area D, Dodoma huku hali yake ikizidi kuimarika kila kukicha.Desemba 26, mbunge huyo alisimama kwa mara ya kwanza na kuanza rasmi kufanya mazoezi ya viungo katika Hospitali hiyo kwa msaada wa madaktari. Lissu anaendelea na mazoezi madogo ya kuimarisha misuli ya miguuni ili aweze kutembea.

Mwanasheria mkuu huyo wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari mara baada ya kufika nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, hivi karibuni alisema bado ana risasi moja mwilini mwake ambayo haijatolewa.

No comments :

Post a Comment