Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), DR.Vincent Mashinji amefunguka na kusema kuwa watu ambao ni wezi wa mali za nchi na waliolipelekea nchi hapa ilipofika kwa mambo mabaya ni baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).Mashinji amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter na kusema kuwa Wazungu hawapaswi kulaumiwa kwani wao walikuja na mapendekezo mbalimbali na viongozi wa CCM ndiyo waliyoyapokea huku akidai chama chake cha CHADEMA kilikuwa kikipinga na wakabezwa.
"Eti Wazungu, wakati wezi ni CCM. Hawa Wazungu wamekuja na mapendekezo CCM ikayapokea kwa mbwembwe na vifijo. Hawakulazimisha, waliridhiana na MaCCM. CHADEMA ikaomba mikataba iletwe bungeni, CCM wakabeza. Mwizi ni nani? Wazungu au CCM? Amkeni Watanzania, adui yupo hapa hapa na si Wazungu" alisisitiza Mashinji.

No comments :
Post a Comment