Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, February 8, 2018

KAMPENI ZA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA HUKO MAREKANI (DMV) ZAANZA KWA KASI KUBWA!

NAOMBA KURA YAKO DJ LUKE FOR DMV PRESIDENT 2018

PLEASE VOTE DJ LUKE FOR  DMV  PRESIBENT 2018

Ndugu mwanajumuiya kwa heshima naomba nichukue nafasi hii kukuomba kura ya ndio katika nafasi ya uraisi kwenye uchaguzi ujao wa wanadiaspora ya Tanzania waishio katika eneo la DMV Marekani.

Jumuiya yetu ina faida nyingi na kuna mengi tunayoweza kuyafanya kwa ushirikiano wako, uongozi na wanajumuiya wote.

Malengo yetu ya awali ni kufanyia katiba marekebisho kwa kuzingatia maoni ya wanajumuiya ikiwa ni pamoja na kutafsiri katiba kwa kiswahili. Tutahakiki usajili wa jumuiya serikalini. Tutapitia vitabu vya mahesabu ya jumuiya na kutoa ripoti zake kwa wanajumuiya kila mwezi. Tutaboresha mawasiliano kwa kutumia tovuti (website) mitandao ya jamii. Tutatumia blogs, redio ikiwemo online redio Kilimanjaro Studio na televisheni za kimataifa (VOA). Tutafanya mikutano ya hadhara na ya ki-electronic.


Tutahamasisha umoja na ushirikiano wa wanajumuiya. Katika hili jumuiya itashirikiana na jumuiya nyingine za DMV kama za kidini, jumuiya za majimbo na nchi nyingine. Jumuiya itaendelea kukusanya michango ya misiba na majanga mpaka tutakapofanikisha kupata njia mbadala.

Tutaandaa mikakati ya kuingiza fedha za jumuiya kwa kutumia misaada ya serikali, michango ya wafadhili na mifuko (foundations) zinazotoa misaada. Vilevile tutaandaa matamasha na shughuli za kukusanya fedha (fundraisers)

Tutafanya sensa ya wanajumuiya wote wa DMV ili tuweze kupanga mipango ya muda mrefu ya uhakika.

Kwa malengo ya siku za baadae tunakusudia kupata ofisi ya jumuiya ili kuweka shughuli za jumuiya kiutaalamu na salama. Jumuiya yetu itatoa huduma katika nyanja mbalimbali zikuwemo uhamiaji, elimu, afya, ajira na ushauri. Jumuiya pia itaandaa utaratibu wa kuwasaidia waliofikwa na misiba na masaibu mengine ya kimaisha. Mkono wa jumuiya hii utafika Tanzania kwa kutumia NGO’s zitakazopeleka misaada.

UHAMIAJI
Jumuiya itaingia ubia na wanasheria wa uhamiaji ili kutoa ushauri na muongozo kwa wanajumuia katika huduma za uhamiaji zikiwemo vibali vya kazi, green cards, uraia na masuala ya kisheria za uhamiaji. Suala la uraia pacha pia tutalipa kipaumbele kwa kupitia ubalozi na serikali ya Tanzania.

ELIMU
Jumuiya itaangalia uwezekano wa kupata scholarships kwa wanajumuiya kwa kupitia mifuko ya misaada ( foundations) Vilevile jumuia Itatoa ushauri na elimu katika masuala tofauti kama masuala ya kifedha, ulipaji kodi, mikopo, ununuzi wa nyumba nk. Suala la watoto wetu halitasahauliwa. Kutakuwa na madarasa ya kiswahili, utaratibu wa shule za watoto (day care), summer camps na mengineyo.

AFYA
Jumuiya itaandaa semina za afya na upimaji wa afya. Mipango ya kuwaelimisha wanajumuiya jinsi ya kupata huduma za bima ya afya kwa bei nafuu pia itafanyiwa kazi. Jumuiya itaandaa vitabu kwa mfumo wa brochures na pamphlets vitakavyotoa takwimu, elimu na kinga za maradhi mbalimbali kama ukimwi, saratani (cancer), shinikizo la damu, kisukari, na mengineyo mengi.

AJIRA
Juhudi za makusudi za kuwaunganisha wanajumuiya wasaidiane na kushirikiana katika kupeana ajira na milango ya biashara zitafanyika. Nafasi za ajira na biashara zitatangazwa kwenye tovuti (website) ya jumuiya na vyombo vingine vya mawasiliano ya wanajumuiya.

USHAURI.
Wataalamu wa fani mbalimbali watakutanishwa na wanajumuiya kwa ushauri. Vilevile baraza la wazee litaanzishwa kusimamia ushauri, usuluhishi na masuala mengine ya jamii.

DMV CARE
Uongozi unaandaa mpango kabambe wa kuwapatia wanajumuiya bima ya dharura za misiba, ugonjwa, kupoteza kazi na mengineyo. Huu utakuwa ni mfuko utakaochangiwa na wanajumuiya kama bima nyingine na una makusudio ya kuwapa wanajumuiya amani ya moyo na faraja wanapotokewa na misiba au maafa mengine ya kimaisha.

Zaidi ya hayo yote jumuiya itaanzisha NGO’s zitakazopeleka misaada Tanzania hasa katika miradi ya afya na elimu.

Mengine zaidi ya hayo yatafuatia kutokana na maoni ya wanajumuiya.

Naomba ushirikiano wako katika kuijenga jumuiya yetu kwa faida yetu na vizazi vyetu vitakavyofuatia.

Wako Mtiifu.

Lucas Mukami


PAMOJA KWA UMOJA TUJENGE DMV MOJA

No comments :

Post a Comment