Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, Raila Amollo Odinga, ametaka kufanyika kwa uchaguzi mkuu mpya tena mwezi Agosti mwaka huu 2018.
Akizungumza na BBC Raila Odinga amesema hamtambui Uhuru Kenyatta kama Rais wa nchi hiyo kwani hana kibali cha watu, ingawa hana lengo lolote la kupambana na serikali ya Kenyatta.
"Hatutamtoa Uhuru Kenyatta Ikulu anaweza kuendelea kukaa kwa amani, lakini hatuutambui Urais wake kwa sababu uko kinyume, tunataka uchaguzi mwingine na kwa mujibu wa ratiba yetu utakuwa Agosti mwaka huu”, amesema Raila Odinga.
Hivi karibuni kiongozi huyo wa upinzani nchini Kenya alijiapisha na kuwa Rais wa watu, akisema yeye ndio chaguo la watu kuwaongoza na sio Uhuru Kenyatta.

No comments :
Post a Comment