Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema inaendelea na juhudi za kusajili wananchi wake wanaoishi nje ya nchi (diaspora) lengo likiwa ni kupata idadi yao kamili.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi ‘Gavu’ alitoa kauli hiyo leo Februari 8, 2018 katika Baraza la Wawakilishi linaloendelea Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, wakati akijibu swali la mwakilishi wa Chumbuni, Miraji Khamis Mussa.
Mussa alitaka kujua pamoja na jitihada za Serikali za kuanzisha kitengo cha wanadiaspora visiwani humo, hadi sasa ni wangapi wamefikiwa na kutambulika pamoja na kupatiwa maelezo halisi juu ya azma ya uanzishwaji wa kitengo hicho.
Gavu amesema pamoja na juhudi kubwa ya Serikali ya kuanzisha idara maalumu inayoshughulikia wanadiapora, hadi sasa hakuna idadi maalumu ingawa kazi ya usajili inaendelea.
Akijibu swali hilo, Govu amesema ingawa suala la diaspora ni la Muungano lakini kwa upande wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi nao wamekuwa na jumuiya zao mbalimbali ambazo zinawaunganisha katika mambo yao.
Gavu amezitaja baadhi ya jumuiya hizo kuwa ni Wazanzibari wanaoishi nchi za Scandinavia (Zandias), Wazanzibari wanaoishi Canada (Zacadia), Wazanzibari wanaoishi Marekani (Zadia), Wazanzibari wanaoishi Uingereza (Zawa), etc.
“Ni wazi kuwa uwapo wa jumuiya hizo katika nchi ni njia moja ya kuongezeka kwa ushirikiana kati Idara yetu ya wanadiapora katika kuhakikisha kuwa idadi halisi ya wanadiaspora wote wa Zanzibar tunaipata,” amesema.

No comments :
Post a Comment