- FIFA na CAF kuendelea kufikiria namna ya kuisaidia Zanzibar
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali serikali iliyozungumza na Marais hao wa mashirikisho ya mpira wa miguu kwa ngazi ya bara la Afrika na Dunia walipofika nchini hivi karibuni kwa ajili ya kufanya mkutano wao wa kuandaa ajenda za mkutano mkuu wa dunia.
‘’Marais hao walisema kuondolewa kwa Zanzibar katika uanachama wa CAF kulizingatia sheria zinazosimamia Shirikisho hilo lakini pamoja na hayo waliamua kuiachia Zanzibar kuendelea kufaidika na fursa zote wanazopatiwa wanachama wa CAF isipokuwa kuwaruhusu kupiga kura, pia wanasema wataangalia zaidi ya hilo maeneo mengine namna ya kuisaidia Zanzibar,''Dkt.Harrison Mwakyembe.
Akiendelea kuzungumza katika Mkutano huo Mheshimiwa Mwakyembe alisisitiza kuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alieleza kwa ufasaha mgogoro huu wa soka kwa viongozi hao wenyedhamana na mashirikisho hayo nao kumuelewa ambapo walisisitiza kuhitaji serikali kuendelea kushauriana nao katika suala hilo.
Pamoja na hayo nae Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia aliwasihi wapenzi wa soka nchini kuendelea kuwa watulivu kwani suala hilo linashughulikiwa na viongozi wa ngazi za juu nao wanalifahamu
No comments :
Post a Comment