Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma, amemshauri waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe kuwapa elimu maalum wasanii badala ya kufungia kazi zao wanapokosea, kwani wanafanya kazi kubwa ya kulitangaza taifa kimataifa.Mbunge Msukuma amesema wasanii wanafanya jitihada binafsi ili kuweza kufanikisha kazi zao zinafanya vizuri, lakini serikali inakuja kufungia kazi zao kwa kigezo cha maadili, jambo ambalo haliingii akilini kwa miaka ya sasa, kwani kupasua nguo kwa msanii ni kitu cha kawaida kwa dunia ya sasa.
Msukuma ameendelea kwa kusema kwamba wanapofungia kazi hizo si sahihi kwani kuna nyimbo za Ulaya nyingi hazina maadili, lakini ndizo wanazozitazama kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii.
“Msanii anafanya kazi nzuri kwenye kushoot akikosea tu kidogo mpasuo Waziri huyo amefungia, sasa mimi nataka kumuuliza, unafungia miziki ya Tanzania, unawafungia wasanii wa Tanzania kuonesha mpasuo, hebu angalia miziki ya kina Rihana, na ndio mnakaa mnaangalia kwenye YouTube humu kila siku, hii ya Tanzania mnataka wasanii wetu wavae dera sijui wavae pekosi, hakuna mtu ana hobi ya miziki ya pekosi miaka hii ya sasa, msanii anafanya kazi nzuri, anainvest pesa ya mkopo, akikosea kidogo mnafunga”, amesema Msukuma.
Mbunge Msukuma ameendelea kwa kusema …."wasanii wetu wanaiga miziki ya Ulaya na wanaiga style za Ulaya, na miziki Ulaya huwezi kupeleka mtu amevaa kanzu au dera, haiwezekani mimi nashauri tuangalie hii faida tunayoipata kupitia wasanii wetu”.

No comments :
Post a Comment