Polisi waliwatia mbarani watu 40 wanaodaiwa kushiriki kwenye maandamano wiki iliyopita nchini Tanzania
Maandamano ya kitaifa yaliyopangwa nchini Tanzania, hayakufanikiwa kutokea leo baada ya Polisi kuwaonya waandamanaji kutoingia barabarani.
Polisi jijini Dar es Salaam imethibitisha kukamatwa kwa watu kumi na moja kwa tuhuma za kushiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika nchi nzima yenye lengo la kupinga utawala wa Rais John Pombe Magufuli.
Hayo yamethibitishwa na kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam Kamanda Lazaro Mambosasa.
"Wawili walikuwa ni wanafunzi wa chuo cha diplomasia na watu tisa walikamatwa katika mtaa wa Samora. Mmoja wao amekutwa akiwa amevaa koti, ambalo ndani yake lilikuwa na bango na alikuwa na tisheti iliyokuwa inashiria kuwa alikuwa akitaka kufanya maandamano.Tukikamilisha upelelezi watafikishwa mahakamani. Hali ya jiji kwa sasa hivi ni shwari."
'Mitaa meupe'
Maandamano hayo yaliandaliwa na mwanaharakati wa kisiasa kwenye mitandao ya kijamii, aliyopo Marekani, Mange KimambiKatikati ya mji wa Dar es Salaam eneo la Posta: ndipo mahali ambapo palisemekana waandamanaji wangekutana, lakini hakuna kilicho tokea
Wakati huo huo, sehemu kubwa ya nchi hasa mijini, ilibaki kimya huku vikosi vya usalama vikionekana kushika doria katika miji mikubwa, hali inayoelezewa kuleta hofu miongoni mwa wananchi.
Kumekuwa na ukimya katikati mwa mji wa Dar es Salaam wakati siku za
kawaida watu hupishana
Siku Jumanne watu 7 walikamatwa kuhusiana na maandamano ya Aprili 26 Tanzania mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania.
Bi Mange Kimambi amekuwa akifanya juhudi za kuandaa maandamano kwa kutumia mitandao ya kijamii, kwa zaidi ya mwezi mmoja.
'Onyo Kali'
Serikali iliwajibu kwa onyo kali.
Mitandao ya kijamii yalivuma na picha na video za vikosi vya askari wakiwa na silaha nzito wakipiga doria katika miji mikubwa Tanzania.
Mkuu wa polisi wa mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto aliwaambia waandishi wa habari kuwa wale waliopanga kufanya maandamano leo wangeshughulikiwa vilivyo.
Rais Magufuli mwenyewe, katika maadhimisho ya muungano kati ya Tanganyika na Zanizibar hakusema lolote kuhusu maandamano hayo, bali kusisitiza Watanzania kuendelea kudumisha amani na wasikubali kutumika kuivuruga amani ya nchi.
'Watu wachache'
Bi Kamambi alishiriki katika maandamano siku ya Jumatano, nje ya ubalozi wa Tanzania mjini Washington, akiwa pamoja na watu wengine waliokuwa wanaomuunga mkono.
Watu wachache walijitokeza katika baadhi ya miji ya Ulaya pamoja na nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Maandamano hayo yalilenga kuipinga serikali ya Magufuli ambayo imeshutumiwa kuzidi kuuminya uhuru wa kujieleza tangu alipoingia madarakani zaidi ya miaka miwili iliyopita.MaoniMaoni
Maoni
Je, kukosa kwa maandamano kufanyika kuna maana gani?
Mchambuzi wa masuala wa siasa Rashid Chilumba, anasema hakutegemea kwa watu kujitokeza kwa wingi kuandamana dhidi ya serikali sababu ya historia ya Watanzania na maandamano.
Anasema watu nchini Tanzania wanatabia ya kuandamana kukiwa na jambo lililowakera katika wakati huo huo, na wakati huo huo wakapata hamasa ya kutoka na kuonyesha makovu yao.
Pamoja na hayo, vitisho vya serikali kusema wangeshughulikia waandamanaji kikamilifu na vikosi vya jeshi kupiga doria iliwatia watu hofu.
Chanzo - BBC
No comments :
Post a Comment