Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 27, 2018

KIONGOZI WA CHADEMA AKAMATWA NA POLISI USIKU WA MANANE!

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Mbeya, George Titho amekamatwa na polisi usiku wa manane nyumbani kwake kijijini Kyimo wilayani Rungwe.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mussa Taibu alipoulizwa kuhusu kukamatwa kiongozi huyo, amesema hana taarifa.
"Sina taarifa hizo, labda nifuatilie lakini jua tu kwamba hali Mbeya ni shwari," amesema Kamanda Taibu.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Boid Mwabulanga amesema Titho alikamatwa usiku wa kuamkia Aprili 26, 2018.

Mwabulanga amesema hawajaambiwa sababu za kukamatwa kwa Titho na jitihada za kumwekea dhamana zimegonga mwamba.

"Walikwenda nyumbani kwake saa nane usiku na kuvunja mlango, wakachukua simu zake kisha wakamchukua kwenda naye kituo cha polisi Tukuyu. Tumekwenda asubuhi kumwekea dhamana lakini walikataa,” amesema.

/ Mwananchi

No comments :

Post a Comment