dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 12, 2018

Korea Kaskazini kusaidiwa kiuchumi na Marekani!

Marekani imesema itaisaidia Korea Kaskazini kiuchumi endapo Pyongyang itaachana na mabomu ya nyuklia.

Hayo yamezungumzwa baada ya Mike Pompeo kufanya ziara nchini Korea Kaskazini.Kwa mujibu wa habari,waziri huyo amefanya mazungumzo ya kina na Kim Jong Un kuhusu uamuzi wa Marekani endapo nchi hiyo itaachana na makombora ya nyuklia.

Hapo awali rais Trump alitangaza rasmi kuwa mkutano baina yake na Kim unatarajia kufanyika 12 Juni Singapore.

Marekani imeahidi kufanya ushirikiano na Korea Kaskazini an Kusini endapo mkutano kati ya Kim na Trump utazaa matunda.

No comments :

Post a Comment