dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 29, 2018

CCM yamuweka hadharani mgombea wake uchaguzi mdogo Zanzibar!

Leo Septemba 29 Kamati Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imempitisha Ramadhani Harlin Chande kuwa mgombea wa uwakilishi wa Jang’ombe katika uchaguzi mdogo  utakaofanyika Oktoba 12.

Taarifa hiyo iliyotelewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole imesema kamati hiyo chini ya Mwenyekiti Rais John Magufuli imeketi leo katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.Katika taarifa hiyo, alisema CCM imerudia kuwaonya wanachama wake wanaokiuka Katiba na kanuni za uchaguzi kwa kuanza kufanya kampeni za chinichini za urais wa Zanzibar.

“CCM imetoa karipio la mwisho kwa wana CCM wanaokiuka Katiba, kanuni za uchaguzi, kanuni za uongozi na maadili kwa kuanza kufanya kampeni za kificho na za wazi za urais wa Zanzibar na kwenda kinyume na utamaduni na desturi njema za chama chetu ambazo kwa pamoja hutuongoza kuwapata viongozi wa CCM na Serikali zake,” imesema taarifa hiyo.

No comments :

Post a Comment