Wajibu wa kupeleka madaraka kwa wananchi ni suala endelevu na linalohitaji ustahamilivu katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Haji Omar Kheir katika ufunguzi wa tamasha la 12 la Asasi za Kiraia, lililofanyia katika ukumbi wa Sanaa, Rahaleo mjini hapa.Tamasha hilo lililowashirki wadau mbali mbali ikiwemo makundi maalum Unguja na Pemba, vijana, wanawake, watu wenye mahitaji maalum na wanafunzi wa Vyuo Vikuu limeandaliwa na Mwavuli wa Asasi za Kiraia Zanzibar (ANGOZA), chini ya Ufadhili wa The Foundation for Civil Society.
Amesema katika kufanikisha azma ya Serikali ya kupeleka madaraka kwa wananchi, asasi za kiraia zina dhima kubwa ya kuhakikisha zinasimama imara na kushinda changamoto zote zinajitokeza katika kufanikisha suala hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Kheir, Naibu Waziri wa Nchi (OR), Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Shamata Shaame Khamis alisema suala la ugatuzi lilioanza kwa majaribio mwaka uliiopita, limekuwa na changamoto kadhaa, hivyo amezitaka Asasi za Kiraia kuchukua nafasi kusaidia juhudi za Serikali kufanikisha azma hiyo.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeea kuweka mazingira bora ili asasi za kiraia ziweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi na bila vikwazo.
Hata hivyo alikemea uwepo wa baadhi ya asasi za kiraia zisizotekeleza majukumu yake ipasavyo, kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake.
“Kuna baadhi na NGO ambazo zimekuwa zikilaumu serikali tu tangu kuanzishwa kwake, hazitekeleza majukumu yake ipasavyo, ni vyema zikaondokana na utaratibu huu, zifanye shughuli zilizofanya kuanzishwa kwake”, alisema Naibu huyo
Naibu Waziri huyo alipongeza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali na Asasi za kiraia nchini na kutaka uendelezwe kwa maslahi ya Taifa na watu wake.
Aidha, alizitaka asasi za kiraia zilizoshiriki katika tamasha hilo kutumia fursa hiyo kujitathmin ili kubaini mapungufu yalijitokeza katika uanzishwa wake pamoja na utekelezaji wa majukumu yao.
Mapema, Mwakilishi kutoka The Foundation for Civil Society Ayubu M. Masaki alisema kutokana na utafiti uliofanyika, imebainika kuwa baadhi ya asasi za kiraia Zanzibar zimekuwa zikikabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo ukosefu wa utawala bora, uhaba wa watendaji, kukosekana kwa umahiri pamoja na ukosefu wa mbinu endelevu za utunishaji wa mfuko.
Alisema awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi inalenga kuimarisha stadi na uwezo wa asasi za kiraia katika kuleta ushawishi na mageuzi ya kisera ili kuleta mabadiliko.
Nae, Mwenyekiti wa ANGOZA, Asha Aboud, akizungumzia kuhusu Tamasha lililopita (2017), alisema miongoni mwa mafanikio yake ni pamoja na ANGOZA kushirikiana na Tume ya Mipango Zanzibar katika kutengeneza MKUZA 111 kwa lugha za Kiiingereza na Kiswahili chepesi, na kubainisha kuwa hivi karibuni unatarajiwa kuchapishwa.
Alisema ANGOZA imekuwa karibu na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa , Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ili kuhakikisha suala la ugatuzi linaeleweka kwa asasi za kiraia na jamii kwa ujumla.

No comments :
Post a Comment