dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 29, 2018

Hizi ndizo sababu za Rais Magufuli kumtumbua Waziri!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameeleza sababu ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Suzan Kolimba ni kuwa kiongozi huyo alishindwa kuwasimamia Wakurugenzi ndani ya Wizara hiyo.

Akizungumza wakati akimuapisha Naibu Waziri mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro Rais Dkt Magufuli amesema wizara hiyo imekuwa haimridhishi kwa namna ambavyo Naibu Waziri aliyepita badala ya kuwasimamia wakurugenzi wa wizara na kusema yeye ndio alikuwa akisimamiwa na watendaji wake.Rais Magufuli amesema "siku nyingi wizara mambo ya nje haijanifurahisha sana mambo yake mengi hayaendi vizuri, Wakurugenzi wake wengi ni dhaifu sana, wizara ile viongozi wake wanatembea sana, sio unakuwa na Naibu Waziri anayeendeshwa na Wakurugenzi badala ya kuwaagiza unachotaka wewe yani wakuongoze, ndio maana niliamua kuwatoa wote Naibu Waziri na Katibu Mkuu wake."

Awali Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassani alionesha kutoridhishwa na namna ambavyo viongozi wa mambo ya nje walivyoratibu moja ya ziara ya viongozi wakubwa waliofika nchini kwa ziara ya kikazi.

No comments :

Post a Comment