Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 27, 2018

Auawa na mume wake na kufungiwa chumbani, mwili wakutwa umeharibika!


Jeshi la polisi mkoani Manyara linamtafuta Baraka Mollel mkazi wa mtaa wa Nyunguu mjini Babati kwa  kumuua mke wake kwa kumnyonga kwa Sweta kisha kumfungia chumbani na kutoweka.

Tukio hilo limetokea Novemba 24 mwaka huu jumamosi majira ya usiku wa kumkia Jumapili .

Kwa mujibu wa Mdogo wa Marehemu Gabriela Mallya aliekuwa akiishi nae amesema  usiku wa jumamosi walikula chakula pamoja na baada ya hapo kila mmoja akaelekea kulala lakini  majira ya saa tano Usiku huo huo mtuhumiwa  aliwagongea watoto akihitaji pochi ya mama iliyokuwa na funguo za dukani kisha akaondoka.

Ameendelea kusimulia kuwa palipokucha kesho yake siku ya Jumapili wakati wanaelekea kanisani majira ya saa 12 asubuhi waligonga mlango ili kuwaaga lakini hawakujibiwa wakaamua kuondoka kuelekea ibadani.

Alisema wakiwa wanatafakari wapi alipo dada Baba,mmoja wa kijana wa karibu na familia hiyo alipokea simu kutoka kwa mtuhumiwa ikimweleza kuwa wapo njiani kuelekea Arusha.

Anasema walipata hofu baada ya kujaribu kuipigia simu ya dada bila ya mafanikio  kwa muda mrefu ndipo walipoamua kumshirikisha kaka yao ambaye aliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Cha Babati baada ya kuuona mwili wa ndugu yao ukiwa kitandani.

Nao majirani wa marehemu wanasema wameshtushwa na taarifa za tukio hilo kwa sababua marehemu alikuwa akitumia muda wake mwingi kufanya biashara zake na hawakuwahi kusikia wawili hao wanagombana zaidi sana wakiwaona ni familia inayoishi kwa ushirikiano.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga akitoa taarifa kwa waandishi wa habari  amemtaja marehemu kuwa ni Josephine Evarest 38  mfanyabiashara mjini Babati.

Amesema kwa mujibu wa Uchunguzi wa kitabibu unaonyesha kwamba mwili huo ulishaanza kuharibika kutokana na kukaa zaidi ya siku mbili ukiwa umefungiwa chumbani.

Kamanda Senga amesema “mdogo wa marehemu alitumiwa ujumbe kwenye simu ya Marehemu,usemao Baba Izack amenipiga”.

Baada ya kutekeleza mauaji hayo mtuhumiwa alikimbia na uchunguzi wa jeshi la Polisi unaonyesha amekwenda mkoa jirani wa Arusha.

No comments :

Post a Comment