Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 27, 2018

Dkt. Shein akutana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa!


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,  Dk. Ali Mohamed Shein  leo  amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia masuala ya Mazingira (UN Environment), Joyce Msuya  katika ukumbi wa  Intercontinenatl Mjini Nairobi, na kulishukuru shirika hilo kwa  kuendelea  kushirikiana na na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar,hasa katika utekekelzaji wa  miradi mbali mbali inayohusu  mazingira na kuwajengea uwezo watendaji.
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa  Rais alisema kwamba  suala la mazingira lina  umuhimu wa pekee katika nchi za visiwa katika wakati huu ambapo, dunia inakabiliwa na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na  athari mbali mbali za kimazingira  zinazosababishwa na shughuli za binaadam.

 Mheshimiwa Rais, alieleza hivi sasa ni vyema ushirikiano  uliopo baina  ya shirika hilo ukazidi kuimarishwa  ili  kuweza kuisaidia Zanzibar katika utekelezaji mpango na miradi ya kutafuta na kuendeleza sekta ya mafuta na gesi asilia.

Dk.Shein alisema kwamba Zanzibar bado haina wataalamu wa kutosha katika kuendeleza na kusimami sekta ya mafuta na gesi na Nyanja mbali mbali zinazogusa sekta hiyo, wakiwemo wataalamu wa mazingira.

 Kwa hivyo, itakuwa ni vyema ikiwa Shirika hilo Iitasaidia Zanzibar katika kuandaa  miongozo, sera na sheria muhimu zinahusu mazingira ili kuweza  kuepuka athari za kimazingira zinazoambatana na sekta hiyo.

Katika kikao hicho,Dk.Shein alisema kwamba Zanzibar imejifunza mambo mengi kutoka katika nchi ambao hazikulipa umuhimu suala la mazingira wakati zilipoingia katika sekta ya mafuta na gesi.

Vile vile, alieleza kwamba itakuwa ni vyema ikiwa Shirika hilo  la Umoja wa Mataifa linashughulikia masuala ya Mazingira litafikiria na kuangalia uwezekano wa kufanyakazi kwa  pamoja na  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kupitia Programu ya pamoja inayojumuisha taasisi mbali mbali za Umoja wa Mataifa zilizopo Zanzibar ambayo aliizindua rasmi mwezi Agosti,  mwaka huu 2018.

 Alifahamisha kwamba, kupitia progarmu hiyo taasisi hizo zimekuwa zikifanyakazi na Serikali katika masuala mbali mbali ya kiuchumi na kijamii kwa ajili ya kuimarisha ustawi wa wananchi wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla,  ikiwemo sekta ya afya, elimu, kujengea uwezo wafanyakazi,  uwezeshaji na mapambano dhidi ya unyanyasaji na udhalishaji wa watoto.

Aidha Dk.Shein alimpongeza kiongozi huyo  Kwa kuchaguliwa kushika  wadhifa huo mkubwa katika ngazi  taasisi ya Kimataifa na kusema kwamba uteuzi aliopata umezingatia uwezo na uzoefu alionao.

No comments :

Post a Comment