Shirika la Reli Tanzania (TRC), limeeleza kushtushwa na maiti ambazo zimekuwa zikiziokota mara kwa mara kwenye njia ya reli.
Limesema kwa wiki iliyopita pekee zimeokotwa maiti mbili kwenye njia hiyo ya reli maeneo ya Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika hilo, Focus Sahani, alisema jana kuwa wahusika walizitupa maiti hizo kwenye reli kama ujanja kuonyesha kwamba watu hao waligongwa na treni.
Alisema shirika hilo limekuwa likiokota maiti kwenye reli hiyo kila mara vitendo ambavyo vinawashtua kwa kuwa hawajui wahusika wanafanya hivyo kwa lengo gani.
"Sasa hivi kumejitokeza matukio mengi tu unakuta wengine wamewekwa relini, watu wanamfanyia mtu kitu kibaya huko wanamtupa kwenye reli ionekane kama amegongwa na treni," alisema.
Alisema maiti hizo hadi sasa hazijafahamika zinatupwa na watu gani kwenye reli.
"Wanaua mtu huko wanamleta kwenye reli wanamuacha hapo ili kuonyesha kuwa amegongwa. Wanafanya hivi ili kuondoa ushahidi wiki iliyopita peke yake tumeokota maiti mbili na matukio ya aina hii yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara," alisema.

No comments :
Post a Comment