zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 10, 2018

Makamu wa Rais: Tunaofanya biashara tulipe kodi!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaomba wakazi wa Tarakea Rombo wale wanaofanya biashara kulipa vizuri kodi kwasababu kodi ndio inaleta maendeleo .

Mh. Samia ameyasema hayo akiwa Tarakea kwenye ziara yake ya siku 5 ambapo amesema kuwa kodi ndio inafanya tufanye maendeleo yote kwasababu wanatumia pesa.

"Hata huku Tarakea kwa macho tu naona biashara imeshamiri vizuri, hasa kwa wale tunaofanya biashara tulipeni kodi ndugu zangu kwasababu kodi ndio inayotufanya tuweze kufanya mengine yote haya kama mnavyojua na mnavyosikia kwamba serikali yenu sasa tunafanya maendeleo yote tunayoyafanya kwa kutumia pesa yetu wenyewe anaekuja kutusaidia hatumfukuzi tunampokea lakini kwanza sisi wenyewe msaada baadae kwahiyo tukikusanya mapato vizuri, " amesema Mama Samia.

Aliongeza "Ndugu zangu tukilipa kodi ndogo ndogo vizuri na hili suala la kodi kuna kodi zenye kuudhi tumepiga marufuku Halmashauri wasitoze, zile zinazouzi wananchi hazitozwi kabisa, lakini zile ambazo tumeruhusu zitozwe tunaomba mlipe".

No comments :

Post a Comment