dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 29, 2018

Masauni Akabidhiwa Orodha ya watuhumiwa Dawa za Kulevya Zanzibar!

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia), akiangalia majina ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao ikiwa ni jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu yaliyoanza kushamiri katika maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar.Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Emmanuel Lukula, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saleh Mohamed Saleh na Katibu wa Naibu Waziri, George Mwansasu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia), akizungumza na wananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja (hawapo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao ikiwa ni jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu yaliyoanza kushamiri katika maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar.Wengine kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saleh Mohamed Saleh na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Zanzibar, Masoud Mabalila. 
Mwananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja, Ally Saleh Ally, akielezea kero ya uhalifu kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia),wakati wa Mkutano wa Hadhara uliokuwa na lengo la kujadili jinsi ya kukomesha matukio ya uhalifu yanayoanza kushamiri Visiwani Zanzibar. 
Mwananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja, Mariamu Said Ali, akielezea kero ya uhalifu kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia),wakati wa Mkutano wa Hadhara uliokuwa na lengo la kujadili jinsi ya kukomesha matukio ya uhalifu yanayoanza kushamiri Visiwani Zanzibar. 
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saleh Mohamed Saleh, akizungumza na wananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja (hawapo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao ikiwa ni jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu yaliyoanza kushamiri katika maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Wananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja wamemkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, orodha ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya Visiwani Zanzibar. Wananchi hao wamekabidhi orodha hiyo baada ya Naibu Waziri Masauni kuwataka waorodheshe majina ya watu wanaowafahamu wakituhumiwa kujihusisha na biashara hiyo ambayo imekuwa ikiaribu nguvu kazi ya Taifa na kusababisha kuwepo kwa matukio ya uhalifu katika sehemu mbalimbali Visiwani humo.

Awali wakiwasilisha kero zao kwa nyakati tofauti wananchi hao waliiomba serikali kudhibiti biashara hiyo ya dawa za kulevya kwani imekua ikishamiri kwa kasi Visiwani humo na wakishangaa ukimya wa mamlaka husika kuacha biashara hiyo ikizidi kuleta madhara katika jamii.
Akizungumza katika Mkutano huo wa hadhara, Naibu Waziri Masauni amewaahidi wananchi hao kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na wauzaji wa dawa za kulevya huku akitoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuwakamata watu wote waliotuhumiwa na uchunguzi uanze mara moja.

“Hatuwezi kama Taifa tukawa na vijana ambao hawana faida katika jamii, vijana ni nguvu kazi ya Taifa, tutahakikisha majina yaliyoletwa hapa tunayafanyia kazi na natoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa na nitahitaji ripoti hiyo ndani ya wiki mbili, haiwezekani watu wachache waharibu nguvu kazi ya Taifa kwa maslahi yao binafsi na familia zao,” alisema Masauni

Akizungumza katika mkutano huo , Kamishna Msaidizi, Saleh Mohamed Saleh, aliwaomba wananchi kuzifikisha taarifa za uhalifu katika vituo vya Jeshi la Polisi au Serikali ya Mtaa ili hatua ziwe zinachukuliwa ili kuweza kudhibiti uhalifu katika maeneo yao.

No comments :

Post a Comment