Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, ameagiza Aisha Hamisi, mzee aliyekaa Hospitali ya Kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida kwa zaidi ya miaka 10, apelekwe kituo cha kuhudumia wazee na wasiojiweza.
Dk. Ndugulile alichukua uamuzi huo jana baada ya kuzungumza na mzee huyo ambaye alimweleza kuwa hana ndugu wala jamaa wa kumpatia huduma muhimu za kibinadamu.
Akiwa kwenye ziara yake hospitali hapo, Dk. Ndugulile alimwagiza Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Rabikira Mushi, kuhakikisha mzee huyo anapelekwa huko ili ahudumiwe kama wazee wengine."Mzee huyu apelekwe makao ya kuwahudumia wazee na wasiojiweza ya Sukamahela iliyopo Wilaya ya Manyoni ili apate huduma muhimu, serikali ina jukumu la kuwatunza wazee na wasiojiweza kwa wale ambao hawana ndugu wala jamaa wa kuwatunza," alisema.
Mushi aliahidi kutekeleza agizo hilo mara moja ili mzee huyo apate huduma muhimu.
Kutokana na uamuzi huo, Aisha alimshukuru Dk. Ndugulile na kumwomba kutatua changamoto za matibabu zinazowakabili wazee nchini.

No comments :
Post a Comment