dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, November 30, 2018

RUSHWA YA NGONO GUMZO CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM....DR SHULE AHUDHURIA KIKAO CHA MAADILI!

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Vicensia Shule amehudhuria kikao cha kamati ya maadili cha chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuwaeleza njia ambazo wanaweza kuzitumia ili kuboresha maadili chuoni hapo.

Katika kikao hicho Dkt.Vicensia amesema kwamba walijadili namna ambayo itaweza kutatua tatizo la rushwa ya ngono lililopo chuoni humo na mpaka sasa hawezi sema muafaka walioufikia kwa sababu yeye aliwasilisha na kuondoka.
Dkt Vicensia alizua mjadala mtandaoni baada ya kudai kwamba rushwa ya ngono imekithiri chuoni humo na kuitwa kufika kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho.

Barua ya kamati hiyo iliyotiwa saini ya mwenyekiti Prof Evelyne Mbede inamtaka mhadhiri huyo kufika mbele ya kamati hiso Ijumaa saa tisa "ili kamati iweze kulifanyia kazi swala hili kwa haraka."

Dkt Vicensia Shule alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba alitaka sana kuufikisha ujumbe wake kwa Rais John Magufuli lakini aliwaogopa walinzi wake.

Dkt Magufuli alikuwa amezuru chuo hicho kufungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwalimu. Julius K. Nyerere) jijini Dar es Salaam.

Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati ilijengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na ndiyo maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika.

Dkt Shule alitaka kutumia bango kuufikisha ujumbe kwa rais huyo.

Aliandika: "Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli."
/ BBC

No comments :

Post a Comment