Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 5, 2018

WACHEZAJI LEICESTER CITY WAWASILI THAILAND KUMZIKA MMILIKI WA KLABU!

Wachezaji wa Leicester City wamewasili nchini Thailand kwa mazishi ya mmiliki wa klabu ambaye alifariki kwenye ajali ya helikopta. Jamie Vardy na nahodha wa klabu Wes Morgan ni baadhi ya wachezaji ambao wamehudhuria mazishi ya Vichai Srivaddhanaprabha kwenye hekalu mjini Bangkok. Mazishi hayo yaliyoanza Jumamosi yataendelea kwa wiki nzima. Helikopta hiyo ilianguka baada ya kupaa kutoka uwanja wa mpira wa klabu hiyo tarehe 27 Oktoba na kumuua Vichai na wengine wanne.
Wachezaji wa Leicester walisafiri kwenda Thailand kwa safari ya saa 12 Jumamosi baada ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Cardiff kenye ligi ya Premier, mechi yao ya kwanza tangu Vichai afariki. Meneja Claude Puel amewangoza wachezaji wake kwenye mazishi hayo.
Nusara Suknamai, Kaveporn Punpare, rubani Eric Swaffer na mpenzi wake, Izabela Roza Lechowicz, nao walikufa kwenye ajali hiyo. Mazishi ya Bi Nusara yalifanyika Bangkok Jumamosi.
Bi Nusara 32 mmoja wa wafanyakazi wake Vichai alichukua nafasi wa pili kwenye shindano la urembo la mwaka 2005 la Miss Thailand Universe.

No comments :

Post a Comment