zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 24, 2018

CCM hawanabudi kuendeleza umoja wao - Balozi Seif!

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi, Balozi Seif Ali Iddi alisema wana CCM hawanabudi kuendeleza Umoja wao utaowapa nguvu za kujihakikishia kuondoza Dola ya Tanzania kwa Miaka mingi ijayo.

Alisema tabia ya baadhi ya wanachama kuhasimiana kwa sababu za tofaurti zao za kuwania uongozi wakati wamchakato wa kuwania nafasi za Uchaguzi ni kutoa mwanya kwa upinzani iwapo hawataamua kuacha makundi yaliyokuwepo wakati wa mchakato huo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo akiwa mlezi Mpya wa Mkoa wa Shinyanga Kichama alipofika kujitambulisha rasmi wakati akizungumza na Uongozi wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kahama na ile ya Mkoa wa Shinganya Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama.Alisema udhaifu  ndani ya Uongozi wa Chama hujichomoza  pale yanapoanza makundi wakati wa mchakato jambo ambalo muongozo wa Chama huridhia hadi pale anapopatikana mgombea Mmoja anayepaswa kuungwa mkono na makundi yote yaliyokuwepo wakati wa mchakata.

Balozi Seif  aliwaeleza Viongozi hao wa Kamati za Siasa za Wilaya ya Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwamba dini zote zimekuwa zikisisitiza upendo na mshikamano unaopaswa kuendelezwa na Viongozi pamoja na wanachama wote wa Chama hicho kikongwe Barani Afrika na Ulimwengni kwa ujumla.

Akizungumzia vita dhidi ya Rushwa, Dawa za kulevya na Udhalilishaji wa Kijinsia Balozi Seif  ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuagiza Uongozi wa Mkoa wa Serikali na Chama kushirikiana katika kuona vita hiyo inafanikiwa vyema.

Alisema kazi hiyo inapaswa kufanywa kwa pamoja na Wabunge waliomo ndani ya Mkoa huo sambamba na kutekeleza ahadi walizotoa kwa wapiga kura wao wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita.

Balozi Seif alisema wao ndio kielelezo cha Chama katika utekelezaji wa majukumu yao, kinyume na hilo utumishi wao hautaweza kuleta afya katika chama, Serikali na Jamii kwa ujumla.

Akikifungua Kikao hicho Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama Nd. Thomas Muyonga alimuomba Mlezi huo wa Chama Mkoa wa Shinyanga kuzifanyia kazi changamoto zinazoukabili Mkoa huo ili utekelezaji wa Ilani uende kama ilivyopangwa.

No comments :

Post a Comment