Jafar Mneke Kaimu naibu katibu mkuu CUF Taifa
Chama cha wananchi CUF kimelaani uminywaji wa demokrasia na uvunjifu wa makusudi wa kanuni na sheria za uchaguzi uliofanywa na wakurugenzi wa Halmashauri na tume ya taifa ya uchaguzi NEC katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Temeke na Kata 48 nchini uliopangwa kufanyika tarehe Jan 19 mwakani.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Taifa, Jafar Mneke alisema katika uchaguzi huo Tume ya taifa ya uchaguzi kuendelea kukiuka taratibu za uchaguzi tena kwa makusudi kwa kitendo cha kuwaengua wagombea wote kutoka katika vyama vya upinzani kwa kushindwa kujaza fomu namba 10 Jambo ambalo sio kweli."Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Temeke amemwodoa mgombea wetu kwa kisingizio cha kutokujaza fomu namba 10 ya maadili ya uchaguzi jambo ambalo sio kweli kwani mchombea wetu alijaza fomu tena mbele ya msimamizi wa uchaguzi" Alisema Mneke.
Alisema mara baada ya kujaza fomu hiyo na kukamilisha kama sheria ya uchaguzi inavyoelekeza alikabidhi fomu hiyo ila tulishangaa tulisoma katika vyombo vya habari kuwa mgombea wetu pamoja na wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani kuwa wameenguliwa katika uchaguzi huo kutokana na kutokujaza fomu za maadili.
Nitoe rai kwa wananchi na wapenda demokrasia kulaani vitendo hivi vya kuhuni ambavyo vimekuwa vikishamili katika chaguzi za hivi karibuni kwani vinaweza kuatalisha amani, umoja na mshikamano uliopo nchini.
Kwa upande wake aliyekuwa mgombea wa ubunge katika uchaguzi huo wa marudio wa jimbo la temeke bw. Mohamed Ngulagwa Alisema kauli iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo si kweli kwani alijaza na kukabidhi fomu na 10 kama inavyotakiwa na sheria ya uchaguzi nchini.
"Nimesikitishwa na taarifa kuwa nimeenguliwa katika uchaguzi huo na wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani hivyo mgombea wa CCM amepita bila kupingwa kutokana na kutokujaza fomu namba 10 ya maadili ya uchaguzi jambo ambalo si kweli na hujuma kwetu" Alisema.
No comments :
Post a Comment