Baadhi ya Wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe Wilaya ya Mkoani Pemba, wakimsikiliza Naibu Waziri, wa Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar, Shadya Mohammed Suleiman, akiwahutubia katika hafla ya kuwakabidhi Sola kwa ajili ya Nyumba zao.
Kaimu Ofisa mdhamini Wizara ya Uwezeshaji , Wazee , Wanawake na Watoto Pemba, Hakim Vuai Shein, akieleza machache kwa wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe Pemba juu ya matumizi ya Sola watakazo kabidhiwa kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo kuzungumza na Wananchi wa Makoongwe.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na watoto Zanzibar, Shadya Mohammed Suleiman, akizungumza na Wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe Wilaya ya Mkoani Pemba , wakati wa hafla ya wakabidhi Sola kwa ajili ya matumizi ya majumbani.
PICHA NA HANIFA SALIM-PEMBA
No comments :
Post a Comment