Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 19, 2018

Hakuna sababu ya kuwawekea masharti wanasiasa wanaohama vyama - Sumaye!


Na. Thabit madai, Zanzibar
Mjumbe wa Kamati kuu ya chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema  ambaye Pia Waziri Mkuu Mstaafu, Fedrik  Sumaye amesema hakuna sababu ya kuwaekea vikwazo na masharti kwa wanasiasa  ambao wana Tabia ya kuhama hama katika vyama vyao vya siasa.

Alisema  wanasiasa hao huwa wanahama kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo vitisho na kununuliwa hivyo kuhama kwao si mapendekezo na matakwa  yao.

“Hakuna sababu ya kuwaekelea masharti maalum wao waache wahame kwani tunajua kuwa kuhama  si mapenzi yao wanahama kwa biashara na sababu nyingine nyingi” alisema Sumaye.

alisema sababu nyingine inayopelekea kwa wanasiasa hao kuhama ni kutafuta vyeo ambavyo wameahidi na upande waohamia.

Waziri mkuu huyo mstafu aliyasema hayo  Jana katika mkutano na vyombo vya habari wakati wakitoa Azimio la  Zanzibar  kufuatia kukaa kwa vyama sita vya upinzani na kuja na Tamko la vyama vya siasa vya upinzani juu ya khatma ya siasa nchini,

Aidha alisema Sumaye alisema Wanasiasa wenye Tabia ya kuhama hama vyama huwa na tabia ya umalya umalaya wa siasa na kusema kuwa wao hawatetereki na tibia hizo na wapo katika kusimamia Democrasia.

Kwa upande mwingine Alieleza kuwa Chama kikuu kinapoanza kununua watu kutoka vyama vingine kutakuwa kimeshafiki mwisho wake hivyo CCMkwa kufanya hivyo kutakuwa kimefikia mwisho wake wa kuongoza.

Kwa upande mwingine alisema wao wapinzani wana amini kuwa watashinda kwani hakuna sehemu yoyote duniani wapigania demecrasia wakashindwa

No comments :

Post a Comment