dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 2, 2018

Polisi wataka Waziri mkuu afunguliwe mashtaka!


Polisi nchini Israel wamependekeza kufunguliwa mashtaka waziri mkuu Benjamin Netanyahu na mke wake Sara kwa madai ulaghai na ufisadi.

Wanashukiwa kuipendelea kampuni ya mawasiliano ya Bezeq telecom ili nayo iweze kuwapendelea kwa kuandika taarifa nzuri kuwahusu.

Bw Netanuyahu alikana madai hayo yanayojulikana kama Case 4000, Mwanasheria mkuu nchini Israel sasa ataamua ikiwa ataleta mashtaka kuhusu madai hayo.

Kwenye taarifa ya leo Jumapili Bw Netanyau alisema: "Mapendezo haya yalifuja hata kabla ya uchunguzi kuanza.

"Nina uhakika kuwa katika kesi hii, mamlaka zinazoangalia suala hili zitafikia uamuzi ule ule kuwa hakuna chochote kwa sababu hakuna."

Mwezi Februari polisi walipendekeza kufunguliwa mashtaka Bw Netanyahu katika kesi zingine mbili za ufisadi.

Ametupilia mbali madai yote kuwa yasiyo na msingi, Vyombo vya habari nchini Israel vinasema kuwa wachunguzi wamemhoji Netanyahu mara kadhaa.

Netanyahu, 69, anaongoza muungano tete lakini anaamini kuwa madai hayo hayawezi kuchochea uchaguzi wa mapema.

Uchaguzi wa bunge unapangwa kufanyika Novemba 19. Bw Netanyahu anahudumu awamu yya pili kama waziri mkuu.

No comments :

Post a Comment