Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 27, 2018

Tundu Lissu afunguka kurudi Tanzania



Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amebainisha kuwa katikati ya mwaka 2019, anaweza kurudi nchini kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake za kisiasa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017.

Mwanasheria huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ametoa kauli hiyo akiwa anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji.

Lissu amesema "katikati ya mwakani naweza kurudi Tanzania, kuanza mazoezi hakutanizuia kurejea kwani naweza kurudi nyumbani na nikawa nakuja Ubelgiji kwa madaktari."

Aidha kuhusiana na kugombea nafasi ya Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 Mwanasheria huyo wa CHADEMA amebainisha kuwa yuko tayari kukiwakilisha chama chake kwenye kinyang'anyiro hicho.

"Wakikaa katika vikao na kunipa bendera ya kukiwakilisha chama changu, nitakubali kubeba msalaba huo mzito kwa mikono miwili" amesema Lissu.

No comments :

Post a Comment