zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 25, 2018

Wanaomiliki silaha kinyume na utaratibu watakiwa kuzisalimisha!



Na Thabit Madai, Zanzibar.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Haji Hassani  amewataka wanaomiliki silaha kinyume na utaratibu na Sheria  kuzisalimisha silaha hizo mara moja kabla ya kuanza msako wa kuwakamata wamiliki hao.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Kamishna huyo alisema hatua hiyo  itasaidia kupunguza matukio ambayo yanaweza kujitokeza kwa watu wanaomiliki kinyume na sheria .

“Wanaomiliki silaha kinyume na sheria na taratibu za nchi wanatakiwa kuzisalimisha mamlaka husika kabla jeshi la polisi halijachukua hatua kali kwao” alisema.

Alisema uwasilishaji wa silaha hizo ni kutokana na sheria  ambari  2 ya mwaka 2015 sheria ya zanziba kifungu  cha 31 , kifungu kidogo cha kwanza, kinachohusu uthibiti wa silaha za moto na miripuko.

Kwa upande mwingine Kamishina huyo aliwaonya wahalifu watakaobainika kufanya    matukio ya kiuhalifu wakati wa sikukuu  za x - mass na mwaka mpya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kukabiliana na wahalifu ndani ya msimu hu wa sikukuuu za x-mass na mwaka mpya” alisema.

Alisema tumeimarisha maeneo yote ya makanisani pamoja na viwanja vya kufurahishia watoto.

No comments :

Post a Comment