Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, January 25, 2019

HILI NI BALAA JENGINE: Familia tatu zalala nje, Zavunjiwa nyumba, Kisa?!


Familia tatu za Mivinjeni Temeke, Dar es Salaam zinalala katika mabanda waliyojijengea kwa muda kutokana na kuvunjiwa nyumba zao usiku wa kuamkia Jumatatu wakiwa wamelala.

Gazeti la HabariLeo lilizungumza na waathirika hao jana mchana ambapo akizungumzia undani wa sakata hilo, mjukuu wa mwenye nyumba, Rajabu Ramadhani alibainisha kuwa wavunjaji hao aliowataja kuwa ni Mgambo wa Jiji waliwasili nyumbani kwao saa 10 alfajiri. Alisema kabla ya kuanza kuvunja nyumba, mgambo hao waliwaomba wanafamilia kutoka nje kuzungumza na kutokana na mazingira kuwa ni usiku walisita kutoka wasijekudhurika.


Alisema ilichukua dakika tano wakiwaita na baada ya kufunguliwa mlango na kuingia ndani bila kujitambulisha walianza kutoa vitu nje huku tingatinga likianza kuvunja kuta za nyumba. Alisema wakati hayo yakiendelea mgambo hao walizima umeme kwenye nyumba kwa kung'oa nyaya bila kutumia weledi ambapo gazeti hili lilizishuhudia nyaya zikiwa zimesambaa chini.

Alisema tukio hilo lilisababisha uharibifu wa vitu vya thamani kama runinga, radio, kuku, bata, ndege, gari walivyokuwa wanavitegemea. "Hii sio haki. Kwanza kesi ipo mahakamani na ni kwa nini waje usiku kuvunja hata hatujaamka sisi tulidhani ni watu wenye nia mbaya kumbe ni watu ambao wanapaswa kutulinda," alisema. HabariLeo liliwakuta wakipanga mabati, matofali, mbao, madirisha huku pembeni ya nyumba yao iliyovunjwa kukiwa na banda la mabati ambalo walisema ndio wanalala sasa.

Pili Rajab ambaye ni msimamizi wa mirathi wa familia iliyoathiriwa na tukio hilo alibainisha kuwa kwa kushirikiana na waathirika wengine, wamewasilisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda wasaidiwe. HabariLeo liliwasiliana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi kuhusiana na suala hilo akasema siku mbili baadaye alitembelea eneo hilo la Mivinjeni na kuzungumza na wananchi mazungumzo ambayo kitengo cha habari cha Manispaa ya Temeke kiliyarusha kwenye mitandao ya kijamii kupitia runinga Temeke Tv.

Mwakabibi alisema eneo hilo lilikuwa na nyumba zaidi ya 90 ambapo wengine wote wameondoka baada ya kulipwa na zilibaki familia hizo nne ambazo alisema fedha za kuwalipa zipo isipokuwa wamekataa kuchukua.

Kuna watu wamemwambia mmoja wa wamiliki wa nyumba hizi, mzee wa miaka zaidi ya 80 kuwa fedha hizo anazopaswa kulipwa ni kidogo na ndio yeye na wenzake wanaendelea kukaa hapa hadi sasa. Pia kuna gereji na yenyewe naipa wiki mbili iondoke,alisema. Mkurugenzi huyo alisema eneo hilo limeshapata mwekezaji na ni moja kati ya maeneo ambayo yanapaswa kuendelezwa.

No comments :

Post a Comment