EARLIER REPORT: https://www.youtube.com/watch?time_continue=2&v=Rw-tunmdkxw
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Damas Ndumbaro pamoja na viongozi wengine wakati wa sherehe ya kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uwanja mkuu wa michezo mjini Kinshasa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Congo imeandika historia mpya kwa kukabidhiana madaraka kwa upendo na ana imani Viongozi wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo na maslahi mapana ya nchi yao.
Makamu wa Rais ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli ameyasema hayo mara baada ya sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Tshisekedi.
“Linalofurahisha ni kwamba ni mara ya kwanza kwa nchi hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya uchaguzi wa kidemokrasia na kukabidhiana madaraka kwa usalama kabisa” alisema Makamu wa Rais.
Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30, 2018, Mhe. Felix Tshisekedi alipata takribani kura milioni 7 sawa na asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa ambapo wagombea wenzake kama Martin Fayulu alipata ailimia 34 sawa na kura milioni 6.4, Bw. Emmanuel Ramazani Shadary alipata asilimia 23 sawa na takribani kura milioni 4.4.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandika historia kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru kwa kukabidhiana madaraka kwa njia ya Amani.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment