dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 6, 2019

PBZ YAPONGEZWA NA PIA YAKUMBUSHWA KUHUSU DIASPORA ACCOUNTS!


Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada, ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association), imetoa hongera kwa Benki ya Watu wa Zanzibar kutokana na kuzindua mfumo mpya wa kutoa huduma za kibenki na kuzima mfumo wa zamani. 

Hatua hio itawahakikishia wateja wa benki hio huduma bora zaidi ya haraka na ya uhakika itakayoondoa kero ya foleni ambayo wateja wakiikabili hasa kwenye mwisho wa mwezi. 

Akitoa hongera hizo wakati akizungumza na blog la ZanzibarNiKwetu, Makamu wa Rais wa Jumuiya hio Bwana Hassan Othman wa Toronto, Canada, pia alisema..." Pamoja na kuwapa hongera Benki ya Watu wa Zanzibar kwa hatua hii muhimu walioichukuwa kuimarisha shughuli zao za kibenki kwa wateja wao, pia tunapenda kuwakumbusha kuwa kwa muda mrefu sasa walituahidi kutuwezesha kufungua Diaspora accounts wakati tupo huku nje, lakini mpaka leo benki yetu hii haijaanzisha huduma hii kwa Wazanzibari wanaoishi nje".


" Diaspora accounts ingeliiwezesha benki kupokea fedha zaidi za kigeni kutoka huku nje, kwani Wazanzibari wengi wenye miradi yao nyumbani wanapendelea kudunduliza nguvu zao kwenye benki za nyumbani kabla hawajaenda".


Aliendelea Bw. Othman kuwa..." Kwa kweli hatufahamu shida ipo wapi. Benki yetu hii hii huko nyuma ilituondeshea shida iliokuwa sugu kwa miaka mingi ya kupeleka pesa nyumbani (remittances) kutoka huku nje". 


"Sote bado tunakumbuka kuwa huko nyuma upelekaji wa pesa nyumbani Tanzania ulikuwa mgumu sana na wengi tukishindwa kutokana na fees kuwa za juu ambazo makampuni ya multi-national conglomerates za remittances zilikuwa zikitutoza, mpaka pale Benki ya Watu wa Zanzibar ilipoingilia kati kutatua suala hili na kutuletea njia yenye bei nafuu kwa kushirikiana na kampuni ya U.K ya WorldRemit".

"Leo tunashukuru, kwani sio bei ni nafuu tu ya kupeleka pesa nyumbani, bali tunaweza pia kupeleka pesa Tanzania bila ya kuenda benki kupanga foleni. Kwahivyo, tunaiomba benki yetu kuwa na moyo ule ule waliotuonesha huko nyuma ili watufungulie hizi diaspora accounts kama walivyotuahidi".


"Kwa huu mfumo wao mpya, sasa hivi ni rahisi kabisa kwa benki yetu kuzianzisha hizi accounts za diaspora bila ya taabu yoyote ile", alimalizia Bw. Othman.


Mwisho, Bwana Othman aliwatakia wafanyakazi wote wa PBZ kila la kheri katika mwaka huu mpya kwenye kazi zao ngumu za kuwahudumia wananchi na kuwakumbusha tena kuwa wasiwasahao wana-diaspora kuhusu ombi lao la kutaka diaspora accounts".

No comments :

Post a Comment