Mkutano uliofanyika jana kati ya Rais Trump na wakuu wa Vyama Bungeni kujaribu kuutatua mgogoro uliolazimisha shughuli za Serikali ya Marekani kufungwa, umeambulia patupu kila upande uking'ang'ania msimamo wake.Mkwamo huo ukiingia siku ya 12 mambo mambo yatachukua sura mpya leo (Alhamis), pale wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watakapofanya kikao cha kwanza mwaka 2019, chini ya udhibiti wa Chama cha Democratic.
Hakuna upande ulioonekana kutetereka katika msimamo wake kuhusiana na bajeti inayotakiwa na Rais Donald Trump ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka baina ya Marekani na Mexico.
Rais Trump amesema atakaidi kuitia saini bajeti yoyote hadi pale matakwa yake ya dola bilioni 5 za kujenga ukuta huo yatakaporidhiwa, na mtu anayetarajiwa kuchaguliwa baadaye leo kuwa spika wa baraza la wawakilishi, Nancy Pelosi, amesema hata ikichukua muda gani, hawatakubali masharti hayo ya Trump.
No comments :
Post a Comment