dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, January 7, 2019

RAIS WA ZANZIBAR MHE. DK. SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA ZURA MAISARA ZANZIBAR!

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo ZURA Maisara Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kulia Waziri wa Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboub Talib, akishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA Maisara, baada ya kuweka jiwe hilo, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika leo, 6-1-2019, katika eneo hilo maisara.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea jengo hilo la ZURA, baada ya hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo hilo, akipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa ZURA Ndg.Haji Kali Haji, kulia na kushoto Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib, akitembelea jengo hilo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa ZURA Ndg. Haji Kali Haji, akitowa maelezo ya michoro ya picha ya jengo hilo haiko pichani wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwekaji wa Jiwe la Msingi, ikiwa ni shamrashamara za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 JENGO Jipya la ZURA Zanzibar linalojengwa katika eneo la maisara litakuwa na gorofa saba pacha. litakapomalizika ujenzi wake unaojengwa na Kampuni ya Kichina ya Hainan International Ltd.
 WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Kichina ya Hainan International Ltd, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakati akihutubia katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la ZURA Maisara Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 Mapinduzi ya Zanzibar.
 WAFANYAKAZI wa ZURA wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo jipya la Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar.

 WAZIRI wa ArdhiNyumba Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib akihutubia wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi wa Jengo la ZURA Maisara Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA Maisara Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Serikali na Wajenzi wa jengo la ZURA.katika picha ya pamoja baada ya uwekaji wa jiwe la msingi.(Picha na Ikulu)


No comments :

Post a Comment