Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 12, 2019

Wasioona Zanzibar waridhishwa na utekelezaji wa agizo la Serikali!


Na Thabit Madai, Zanzibar
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wasioona Wilaya ya kati Unguja Yusus Kassim amesema wamefurahishwa na matokeo mazuri ya utekelezaji wa maagizo yao waliyoyapeleka katika Serikali ya Halmashauri ya Wilaya ikiwemo kurekebishwa miundombinu ya shule kwa wasioona.

Kassim amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari akitaja baadhi ya mafanikio ya mradi wa uwajibikaji unaotekelezwa na mradi wa PAZA unaozihusisha Serikali za mitaa.

Alisema kabla ya kuanza kwa mradi wa PAZA mwaka mmoja, miundombinu ya shule nyingi ziliopo wilaya ya kati ilikuwa imeharibika na kusabaisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kuona.
Kwa mfano alisema zaidi ya wanafunzi 10 walilazimika kuacha shule kwa sababu miundo mbinu iliopo shule haikuwa rafiki na kuweza kufikiwa kwa urahisi na wanafunzi hao pamoja na vifaa vya kufundishia.

''Nimefurahishwa na utekelezaji wa mradi wa uwajibikikaji ambao umewawezesha viongozi wa halmashauri za wilaya kuwajibika na kutekeleza majukumu yao vizuri katika kutoa huduma kwa wananchi''alisema.

Mradi wa kukuza uwajibikaji (PAZA) unatekelezwa na chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA kwa kushirikiana na jumuiya ya waandishi wa habari za maendeleo (WAHAMAZA) pamoja na jumuiya ya msitu wa wa Ngezi Pemba (NGERANECO) na kufadhiliwa na jumuiya ya Ulaya.

No comments :

Post a Comment