ZACADIA - Zanzibar Canadian Diaspora Association, imetoa mfumo mpya wa kuchangia kwa wana-jumuiya wake.
Katika ujumbe uliosambazwa kwa wana-jumuiya kupitia emails na WhatsApp ambao ZanzibarNiKwetu ulibahatika kuupata, Zacadia imetaja kwanza majukumu yake ya mwaka 2019 kwa kuandika"...Majukumu yetu makubwa ya Zacadia tuliyojiwekea kwa mwaka huu wa 2019 ni pamoja na kuendelea kuwatizama mayatima wetu waliopo Pemba na Unguja kihali na mali, hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao kwa sasa haupo mbali".
"Pia, tunaendeleza kwa mwaka huu wa 2019 majukumu ya kusaidia nyumbani kwa kupeleka vifaa tafauti katika hospitali na shule zetu. Kama tunavyojua tayari tushapeleka nyumbani wheelchairs zaidi ya 60, textbooks zenye thamani ya zaidi ya bilioni 3, vitanda, walkers, etc....."
Ujumbe huo uliosambazwa kwa wana-jumuiya tu uliendelea...."Huko nyuma tulikubaliana kila mtu kutoa kila mwezi Dollar 20. Dollar 20 kwetu kwa wengine kwa miezi miengine inakuwa ni ngumu kutokana na maisha ya leo, lakini lililokuwa gumu zaidi ni ukusanyaji wa hizi pesa. Kumpata mtu kila mwezi akawa anawakumbusha wana-jumuiya inakuwa ni usumbufu na kuipa instruction benki yako ipeleke ZACADIA Dollar 20 tu kila mwezi pia inakuwa uzito kwa wengi".
"Kwahivyo basi, sasa tunakuja na mfumo mpya wa kukusanya hii michango ya kila mwezi. Mfumo huu ni sawa na ule wa gofundme, isipokuwa huu ni kuwa unaji-commit amount fulani na kila mwezi amount hio inatoka kwenye credit card yako. Mfumo wenyewe ni ule wa PAETRON. Ukitaka kuchangia bonyeza hapa:
https://www.patreon.com/zacadia
https://www.patreon.com/zacadia
"...Pesa zote zitakuenda moja kwa moja kwenye Zacadia bank account kwenye benki yetu ya BMO. Kila tunapokuwa na mkutano tutakuja na printed statement kutoka benki kuonesha kiasi gani tumepokea, kiasi gani zinaingia kila mwezi na hakiba yetu yote ni kiasi gani. Hesabu zetu zote kama desturi yetu zitakuwa wazi kwa yoyote yule anaechangia. Mwanachama anaechangia anayohaki wakati wowote ule yakuona statement ya hakiba yetu benki, ili aone maendeleo ya michango yake".
Ujumbe huo uli-define nani kuanzia sasa atakuwa Mwana-Zacadia na nani atakuwa sie.
"Wanachama wa Zacadia watakuwa ni wale tu wanaochangia kila mwezi at least Dollar 5. Tutakapoitisha mikutano na tutakapotoa habari zozote kuhusu Zacadia au kutoka nyumbani, basi tutakuwa tunawasiliana na wanachama wanaochangia tu. Kama mtu hachangii kila mwezi basi huyo atakuwa hayupo kwenye list ya Zacadia na kwahivyo tutakuwa hatumjui. Kwa njia hii tunajua kuwa idadi ya wanachama wetu itapungua, lakini tunahisi ni bora kuwa na wanachama wachache ambao wapo committed to the objectives of our organization kuliko kuwa na wanachama wengi ambao hawapo committed kihali na mali".
Ujumbe huo ulieleza kuwa...."Uzuri wa njia hii ya kuchangia ni kuwa hata marafiki zetu waliopo nje, kama vile Oman, UAE, Europe, etc wanaweza kuchangia, kwani huko nyuma walikuwa wakichangia kwaajili ya watoto wetu mayatima na kwahivyo tuwajulishe na tuwapelekee link hii:
https://www.patreon.com/zacadia"
https://www.patreon.com/zacadia"
"Tuwajulishe marafiki zetu wa ndani na wa nje pamoja na jamaa zetu. Pia, tuwajulishe Wana-Zacadia wenzetu na wasiokuwa Wana-Zacadia, kwani hili ni jambo la kheri katika kujenga akhera yetu", ulimalizia ujumbe huo.
No comments :
Post a Comment