
Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imetoa ushauri kwa Serikali kuandaa na kutekeleza mpango mkakati chini ya Magereza kuwafanya wafungwa wanapata haki ya tendo la ndoa.
"Serikali iandae na kutekeleza mpango mkakati chini ya Magereza ambao utahakikisha wafungwa wenye ndoa wanawekewa mazingira yatakayohakikisha wanapata haki ya kutembelewa na wenzi wao na kupata haki ya tendo la ndoa kwa kuzingatia utaratibu utakaowekwa na mamlaka husika,"amesema Mwenyekiti wake, Mohamed Mchengerwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mchengerwa wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kamati hiyo bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa Februari 8, 2019 ambapo amesema hatua hiyo itapunguza maambukizi ya magonjwa kwenye magereza.
No comments :
Post a Comment