Na Thadei Ole Mushi.
Due diligence ni utafiti unaotafuta ukweli kuhusu uwezo wa mtu au kampuni kibiashara (Operational meaning).
Process hii ya kuchunguza au kutafiti uwezo wa mtu au Kampuni huusisha kupitia financial records, Financial statements kama vile kujua mtu huyo au kampuni hiyo benki wana Shilingi ngapi na mzunguko wao wa fedha upoje.
Mara nyingi Due diligence hufanywa na mtu ambaye anataka kuingia ubia na mtu mwingine kibiashara au kampuni moja kutaka kuingia ubia na kampuni jingine. Wote wawili wanafanya Due diligence kujiridhisha kama kweli partner wako ana mtaji wa kutosha.
FACT.
Ni jambo la kushangaza organ (Serikali nzima) kuzidiwa ujanja na mtu mmoja. Yaani Zitto kabwe ana uwezo kuliko Baraza zima la mawaziri kwa kuona na kunusa ubabaishaji wa Indo Power. Serikali ina kila kitu katika kurahisisha upatikanaji wa taarifa, serikalini kuna vyombo lukuki, tuna maofisa kibao pale Kenya kwenye ubalozi wetu ambao wangeweza kutupa taarifa za hawa Indo Power.
Zitto yeye alijulia wapi kuwa hawa Indo hawana uwezo? Ni kwa sababu zitto ndiye mbunge anayesoma mambo mengi kuliko wabunge wote wa CCM pale Bungeni. Mtaji wa wabunge wetu ni kiganja kama cha baunsa kinachoweza kutandika makofi madesk ya pale Bungeni.
Kama tukipata wabunge kama zito 50 tu pale Bungeni nchi hii ingesonga sana. Niliwahi kuandika kuwa Wabunge wa Upinzani wanalisaidia sana taifa hili kuliko wabunge was CCM ambao hawajui chochote.
Hawajui kwa sababu wala hawatafuti kujua hili la Indo Power limewarudisha wapinzani kwenye mstari kuwa tulisema. Wabunge wetu wa CCM wanahitaji semina elekezi sana namna ya kujiposition na kutafuta maarifa.
Tunahitaji kuwekeza kwa watu SMART, ubunge si kugonga meza tu kwa miaka 5. Naangalia wabunge wangu wa CCM wameweza kusimamia agenda gani ya muhimu kwa miaka hii mitano sioni kitu.
Tuachane na swala la kujua kusoma na kuandika kuwa kigezo cha kugombea ubunge, dunia imebadilika na siasa inatumika kama uchochoro wa kupitishia dili za kiuchumi. Ni lazima tuwe na aina ya wabunge wanaoweza kutafuta taarifa, wanaoweza kutafsiri matukio na wanaoweza kusimamia maslahi ya taifa.
Kabudi hapa alizidiwa ujanja kwa mbali sana na kijana Zitto. Zitto ni Smart kuliko mzee Kabudi. Tujifunze pia kusikiliza ushauri wa wengine.
Ni aibu kusema mlifanya Due Diligence kwa kuangalia mteja alikuja na ndege ya kukodi. Kabudi alidai kuwa Indo walikuja kwa ndege ya kukodi hivyo alijiridhisha wana uwezo wa kununua Korosho. Kuna tifauti gani kati yao na Kangomba mliowafukuza kule mtwara? Kweli Due Diligence inafanywa hivyo? Kwa kuangalia mavazi ya mtu?...Ni mambo mangapi tumeshikishwa kwa uzembe kama huu?
Sioni haja ya CCM kusimamisha mgombea Pale Ujiji.... Wamwache tu Zitto aendelee kuwa mbunge pale. Itakuwa ni ujinga wa kiwango cha SGR kama tutasimamisha mbunge pale yaani tumtoe Zitto Bungeni tuwaongeze wazee wa makofi na ndioooo.
Hizi akili za Zitto ni Mali ya Rais tusiziache zizagae mtaani. Tuzitumie kupiga hatua Mbele....sijui CCM tunakosea wapi tunajikuta wabunge wetu wote wanalingana kiakili.
CCM isiruhusu kila mtu kugombea Ubunge kupitia CCM, Kuwepo na procedure za ndani za kutafuta vichwa watakaokamata form. Vinginevyo kila Siku Zitto atakuwa anatuburuza pale Bungeni....
Ole Mushi
0712702602
No comments :
Post a Comment