Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, May 23, 2019

Waziri Mkuu Uingereza ahofia mgawanyiko kama bunge litapinga mpango wa Brexit!

 Waziri Mkuu wa Uingereza anayekumbwa na shinikizo Theresa May amewaonya wabunge kuwa "mpasuko na mkwamo" huenda vikawafuata, kama watakataa tena mpango wake wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, wakati akikabiliwa na uwezekano wa kuangushwa kwa mara ya nne bungeni.

May amewaambia wabunge wakati akiwasilisha mpango wake huo uliopitiwa upya wa Brexit kuwa nchi hiyo inakabiliwa na kitisho cha kuondoka Ulaya bila ya makubaliano, kitu ambacho bunge na watu wa Uingereza hawawezi kukubali kamwe.
 May amesema amefanya marekebisho baada ya wabunge kukataa mpango huo mara tatu wakati kukikuwa na upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa upinzani na wengi wanaoelezea mashaka katika sera za Ulaya ndani ya chama chake cha Conservative.

Amemuandikia barua kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Jeremy Corbyn akimtaka kuunga mkono mswada huo mpya.

No comments :

Post a Comment