Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 28, 2019

RC Ayoub awapa ushauri wahitimu wa madarasa ya itikadi!

Mjumbe  wa kamati ya siasa ya Mkoa wa Magharibi kichama Ayoub Mohammed Mahmoud amewashauri wahitimu wa madarasa kiitikadi kutumia vyema mafunzo waliyapata kwa maslahi ya Chama cha Mapinduzi CCM na Nchi kwa Ujumla.

Aliwaambia  wahitimu hao  kuwa madarasa ya itikadi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ni nyenzo moja wapo ya kuwaunganisha pamoja wanachama wao kwa lengo la kuwa pamoja kiitikadi.

" madarasa haya yana lengo la kuwaunganisha mume wamoja na kuwa nyenzo ya Ushindi wa Chama chetu ifikapo 2020" alisema Mjumbe huyo.
Mjumbe huyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja aliyasema hayo katika Mahafali ya   madarasa ya Itikadi katika wilaya ya Mfenesini Unguja,

alisema kuwa umoja na mashirikiano ndani ya chama cha mapinduzi ni moja ya nyenzo ya kuimarisha chama hicho na kuhakikishia Ushindi wa mapema kabla ya kufika 2020.

Alisema chama cha mapinduzi kimeamua kuwafunza itikadi vijana wanaochipukia ili watambue historia ya nchi yao ili kukuza mapenzi ya chama na viongozi wake hivyo wahitimu hao wanapaswa kuwa mabalozi wazuri kwa kukisemea vyema chama na serikali zao.

Alisema iwapo vijana hao na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo watashirikiana kuelezea mafanikio yaliyopatikana kupitia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho, watasaidia kujenga uelewa wa jamii na kuwavutia kuendelea kukiunga mkono.

Aidha ayoub ambae pia ni mkuu wa mkoa wa mjini magharibi amewaasa viongozi wenye watu wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2020 kuacha kufanya hivyo badala yake washirikiane na viongozi waliopo kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2015 – 2020 na kwamba hatosita kutoa taarifa zao katika vikao halali vya uteuzi wakati utakapofika.

Katika hatua nyengine ayoub alipongeza ushirikiano uliopo kati ya chama cha mapinduzi wilayani humo na wilaya ya kinondoni Dar es salam ambao alisema utasaidia kuimarisha muungano wa Tanzania lakini pia kujifunza mbinu na mikakati mbali mbali ya kukiimarisha chama katika wilaya hizo.

Akizungungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni aliwasihi vijana kuwa na mapenzi ya kweli kwa chama chao na kukipigania ili kiendelee kushika dola katika pande zote mbili za muungano.

Alisema waasisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania waliweza kupigania uhuru na kuzikomboa nchi mbili hizi kutokana na kuwa na itikadi ya kweli kwa chama nanchi yao jambo linalotakiwa kuendelezwa na kila mwanachama wa CCM bila ya kujali cheo au dhamana aliyonayo.

Akisoma taarifa kuhusu masomo hao katibu wa ccm jimbo la bububu zaituni tawakal khairallah amesema katika mafunzo hayo ya miezi mitatu jumla ya vijana 600 wanawake 420 na wanaume 180 walipatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo.

Alisema vijana hao kutoka matawi manane yaliyomo katika jimbo hilo, walifundishwa historia, itikadi na uzalendo jambo lililowaongeza uwezo wa kujitambua, ujasiri na uzalendo kwa nchi na chama chao.

Katika mahafali hayo wahitimu hao walikabidhiwa vyeti na kadi za uanachama wa CCM na mkuu huyo wa mkoa ambae pia aliahidi kutatua baadhi ya changamoto za jimbo hilo ikiwemo ya vifaa ofisi.

No comments :

Post a Comment