Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uingereza Jeremy Corbyn amesema atawaamuru wabunge wa chama chake wayapinge mapendekezo mapya juu Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Boris Johnson.
Bwana Corbyn amesema mapendekezo hayo hayazingatii hali halisi na yataleta madhara. Corbyn ameeleza kuwa hata Waziri Mkuu mwenyewe anatambua kwamba mapendekezo hayo yatapingwa na Umoja wa Ulaya lakini Waziri Mkuu Johnson amezipinga lawama hizo na ameeleza kuwa serikali yake imefanya juhudi za dhati kuondosha mkwamo katika mchakato wa Brexit huku muda ukiyoyoma kufikia mwishoni mwa mwezi huu ambapo Uingereza inatarajia kujiondoa Umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk ameandika kwenye Twitter kuwa Jumuiya hiyo inasimama thabiti na Jamuhuri ya Ireland lakini pia amesema Umoja huo haujaridhishwa na mapendekezo mapya ya bwana Johnson.
No comments :
Post a Comment