WAISLAMU HUENDA SOTE AU BAADHI YETU TUNAFAHAMU KUWA SIKU YA KIAMA TUTALAZIMIKA KUVUKA DARAJA LA SIRAATH. INSHA ALLAH LEO TUTAFAHAMU ZAIDI KUHUSU DARAJA LA SIRAATH??
Bila Shaka sote waislamu twafahamu kwamba Allah Subhana Wa Ta’ala Ameshahukumu kwamba ili kila mmoja wetu aingie JANNAAH, basi ni lazima alivuke hili daraja la SIRAATH...
JEE DARAJA LA SIRAATH LIMEUNDWA VIPI?
*Ni daraja ambalo litaekwa juu ya moto mkali wa Jahannam na kila mmoja wetu atawajibika alipite kuelekea Jannah.....
*Ni daraja lenye utelezo mkali...
*Ni daraja Nyembamba zaidi ya unywele...
*Ni daraja lenye makali zaidi ya mkuki ulionolewa.....
*Ni daraja lilopambwa kwa miba mirefu mfano wa hooks(ndoano).
KUVUKA KTK DARAJA HILI KUTATEGEMEA MATENDO YAKO HAPA DUNIANI.
*Kumbuka kuwa wapo watakaopita kwenye daraja hili kwa haraka mno mfano wa upepeso wa jicho(twinkle of an eye) na kuifikia Jannah..
*Wengine wataipita kama umeme na kuifikia Jannah..
*Wengine watapita mfano wa nyota yenye kuanguka..
*Wengine kama farasi..
*Wengine watatambaa kama watoto wachanga (Subhana Allah)..
*Wapo watakaoipita bila kudhuriwa kwa ile miba.
*Wapo pia watakaopita na kuivuka baada ya kukwangurwa na kujeruhiwa.
*Na wapo ambao hawatofanikiwa kufika upande wa pili, upande wa Jannah.
*Wapo wengine hawatajua kama wameshaipita siraath kwa sababu ya ile speed kali walotumia kuipita, Na kwa mshangao, watawauliza Malaika: "ziko wapi siraath na Jahannam, tumezipita kweli?"
Malaika watawaambia:
"ndio, mumeivuka siraath ambayo ilikuwa juu ya Jahannam"
Hao ni wale walokuwa na matendo mema humu duniani
Usisahau kauli ya Allah Subhana Wa Ta’ala kwamba "lazima kila mmoja wetu ataifikia siraath"....
Jee Ndugu zangu, tumejiandaa vipi kulivuka daraja hili lenye utelezo na miba? Njia ambayo ni nyembamba zaidi ya unywele na lenye makali zaidi ya mkuki?
Kakangu dadangu ishi utakavoishi lkn kumbuka hili daraja linakusubiri.
Fanya ufanyayo lkn kumbuka hili daraja linakusubiri.
Allah Subhana Wa Ta’ala Atujaalie tulivuke kwa wepesi. Ameen
No comments :
Post a Comment