Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ameshindwa kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi inayomkabili ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli kwa sababu gari lake limepata hitilafu akitokea Dodoma kuja Dar es Salaam.
Hayo yamebainika mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya usikilizwaji wa shahidi lakini mshtakiwa hayupo Mahakamani.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba alimtaka mdhamini wa Mdee, Fareson Rukomo kuielezea mahakama hiyo kwa nini Mbunge huyo hajafika ndipo alidai kuwa gari lake limeharibika kati ya Dodoma na Morogoro wakati anakuja DSM na kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba ameahirisha shauri hilo hadi Novemba 8, 2019 itakapokuja kwa ajili ya usikilizwaji.
Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa kuwa kati ya July 3, 2017 maeneo ya Ofisi za CHADEMA zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Dar es Salaam ambapo anadaiwa alimtukana Rais Magufuli kwamba “anaongea hovyohovyo anatakiwa afunge break”, kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

No comments :
Post a Comment