Israel imeliapisha bunge lake jipya hii leo kwa kile kinachoonekana kuwa muda mfupi baada ya uchaguzi ya pili mwaka huu ambao haukutoa majibu ya kuundwa serikali mpya.
Hafla hiyo ambayo kwa kawaida ni ya sherehe, imeandaliwa sambamba na vikao vya kesi dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuhusu mashtaka ya ufisadi ambayo yametishia kuhitimisha kazi yake ya kisiasa na kuchangia katika mkwamo wa mfumo wa kisiasa nchini humo.
Netanyahu na mpinzani wake mkuu Benny Gantz wote wameshindwa kupata wingi wa viti bungeni na vyama washirika wao.
Sasa wanategemeana kuunda serikali ya muungano kama chaguo la pekee la kuepuka uchaguzi wa tatu jambo lisilo la kawaida kufanyika katika muda wa chini ya mwaka mmoja.

No comments :
Post a Comment