Marekani inajiandaa kuziwekea ushuru bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 7.5 zinazotoka Umoja wa Ulaya, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi ruzuku isiyo halali ya umoja huo kwa kampuni inayotengeneza ndege ya Airbus.
Tangazo hilo limetolewa saa kadhaa baada ya Shirika la Biashara Ulimwenguni, WTO, hapo jana kutoa hukumu ya kesi iliyodumu kwa miaka 15, kwamba Marekani inaweza kuziwekea ushuru bidhaa za Ulaya ili kulipiza kisasi ruzuku hizo kwa Airbus ambazo zimekuwa na athari kwa mpinzani wake nchini humo, Boeing.

Kulingana na ofisi ya mwakilishi wa biashara wa Marekani, nchi hiyo inapanga kuweka ushuru wa asilimia 10 kwenye ndege zinazoingizwa kutoka Ulaya na asilimia 25 ya kodi za bidhaa za kilimo na viwanda zinazoingizwa nchini humo ifikapo Oktoba 18.
WTO ilipitisha kiwango cha ruzuku kwa asilimia 100, lakini Marekani iliamua kuweka ukomo.

No comments :
Post a Comment