Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 4, 2019

Orodha ya watu 10 ambao historia zao zimeleta mchango mkubwa sana duniani!

Historia haikuweki wala kukutambua kuwa na akili sana kwa wingi wa maswali uliyojibu kwenye darsa la hesabu. Albert Einstein alifukuzwa darasani mara nyingi sana sababu mwalimu wake alidhani kuwa ni kichaa.. Newton alionekana ana matatizo ya kujifunza, na walimu wakampeleka kwenye shule maalum. Hata muigizaji maarufu Holliwood Tom Cruise, alionekana hana uwezo wa kujifunza vizuri darasani. Watu wote hawa bado waliweza kufanya mambo makubwa hadi wakaweka alama zao kwenye uso wa dunia.

Ugunduzi wa kisayansi umesaidia dunai kuwa hapa ilipo leo hii, ukianzia kwa kina Newton hadi kina Einstein na wengine kibao.

Hii hapa orodha ya watu 10 ambao historia zao zimeleta mchango mkubwa sana dunaini hadi kesho;

ALEXANDER THE GREAT
Alikua kijana mdogo alipewa madaraka ya kuingoza nchi ya Macedonia, na baba yake akiwa na miaka 16, aliweza kuongoza na kutawala nchi nyingi za bara la Asia. Alionekana mwenye akili na utashi wa uongozi  kwa kuiwezesha Macedonia kuitawala  alipopewa madaraka na baba yake. Alexander alifariki kwa kuumwa malaria.
MICHEL ANGELO
Tofauti kati ya kazi ya sanaa ya Michel Angelo na Da Vinci, imeikita kwenye mitindo mbalimbali ya usanii wao wa uchoraji. Japo wote hawa ni wasanii wakubwa na wana mchango mkubwa sana kwenye sanaa ya uchoraji. Michel Angelo aliwahi kuwa mchoraji mkubwa na alikua akichora sana kwenye siling board.

THOMAS EDISON
Mgunduzi wa wa bulbu ya umeme, alikua akifanya kazi zake na Nicolas Tesla, japo mwisho wa kazi bulbu zilikua mali yake. Edison ni mtu ambaye inabidi umshukuru sana kila ukiwasha taa (bulbu).

LEONARDO DA VINCI
Ukiwa una muongelea Leonardo, unaweza kujiuliza sana maswali juu yake, je alikua mtu gani, msanii, wanasayansi , Mwanamitindo, mchambuzi, ama mchoraji ?. Jibu linabaki kuwa Leonardo alikuwa anauwezo wa kufanya yote hayo. Mchoro wake maarufu ulikua ule wa Mona Lisa, Pia yeye ndio alichora mchoro wa helkopta/ndege kwa mara ya kwanza.

WILLIAM SHAKESPEARE
Binadamu alikua amejaliwa vipaji vingi sana,. Shakespeare ni miongoni mwa watu waliokua na mchango mkubwa sana kwenye ulimwengu wa sanaa ya uandishi. Aliweza kuandika vitabu ama tamthilia 36, Shakespeare ni miongoni mwa waandishi wakubwa waliowahi kutokea duniani. Uwezo wake wa kufikiria kwa mitazamo tofauti tofauti, ndio umempa nafasi hiyo ya kuwa Shakespeare.

ADOLF HITLER
Unaweza kujiuliza kwanini amefanikiwa kuingia kwenye orodha ya watu 10 mashuhuri zaidi duniani.
Adolf Hitler ndio mwanaume peke yake ndio anahusika kwa vifo vya mamilioni ya watu duniani. Kwa kuanzisha chama cha Nazism nchini ujerumani, aliwaongopea dunaini nzima, kwamba alikua sahihi na mitazamo yake, ndipo alipoanza uuwaji wa watu wenye asili ya Israeli. Adolf Hitler alikua na asili ya Israel kwani baba yake alikua na asili ya Israeli, baadae baba yake aliwatenga yeye na mama yake.

GALILEO GALILEI
Mwanadamu ambaye alitupa uwezo wa kuona juu ya anga kwa kutumia Darubini/Hadubini, ambayo iliwapa watu uwezo wa kugundua uzuri na siri za anga. Ugunduzi huu wa Galileo, umeweza kusaidia sana mambo mbalimbali kuanzia maendeleo ya jeshini, na hata wana anga, kama NASA, ambao bila ugunduzi wa Galileo pengine kusingekua na NASA

STEPHEN HAWKING
Ni mtu alikuja kufanya kazi ama kumalizia kazi za Einstein kwani aliweza kuzifanyia utafiti kauli, na mitazamo pamoja na mawazo na kuifanya kuwa kweli. Einstein alikua anatoa mawazo mengi sana ambayo akili ya kawaida ilikua haiwezi kuyafikiria. Stephen alisahihisha na kuweka usawa kuwa kipingamizi kikubwa ni akili ya mwanadamu mwenyewe, na sio uwezekano, hivyo akili ndio inayoizuia kukubali ukweli na kuendelea kukaa nyuma.

ISAAC NEWTON
Mtaalamu wa hisabati na sheria za kisayansi, Isaac ameweka usawa kwenye somo la fizikia, ambayo hutumia kila siku. Mawazo ya Isaac ambayo hueleweka hata kwa watu wa kawaida. Kwenye sheria nyingi za sayansi ama mvutano. Lakini Isaac ndiye ametupa sheria za uvutano na mwendo duniani / Laws of Motion and Gravity.

ALBERT EINSTEIN
Inawezekana wote tunamjua Albert Einstein ni mmoja wa watu waliokua na akili sana kuwahi kutokea duniani. Inasemeka kuwa akili ya Albert ilikua inafanya kazi mara 4 zaidi ya akili za watu wa kawaida. Albert Einstein ni miongoni mwa wanasayansi wanaofahamika sana na wenye mchango mkubwa sana kwa karne ya 20. Jina la Einstein limebeba utambulisho wa pekee, hata mtu anayeitwa jina la Einstein huwa ana aminika kuwa na uwezo mkubwa sana wa akili, tena na ubunifu mkubwa usioisha.

No comments :

Post a Comment