Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 2, 2019

IGP Sirro amtaka kijana aliyetishia bastola kuripoti polisi!!



By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amemtaka kijana aliyemtishia mwenzake bastola kuripoti polisi baada ya kuonekana akifanya kitendo hicho katika picha za video zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.

Mbali na kuripoti, Sirro amesema anatakiwa kusalimisha silaha yake.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla ya uzinduzi wa kampeni ya Utatu inayolenga kukomesha rushwa barabarani.


Sirro amesema ameagiza kukamatwa kwa kijana huyo lakini amekuwa akipiga chenga, amemtaka akajisalimishe mwenyewe kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani.

"Sisi tunatoa vibali vya silaha vinavyoambatana na masharti yake. Mtu anayepewa kibali cha kumiliki silaha lazima akidhi masharti hayo," amesema Sirro.

Amesema licha ya kutojua chanzo cha ugomvi lakini kijana huyo hakutakiwa kuwatishia wenzake kwa silaha,” atakaporipoti atahojiwa zaidi kujua undani wa tukio hilo.”

No comments :

Post a Comment