"Nchi Inaangamia Viongozi Hawana Maarifa na Hawataki Wakosolewe Wanafanya Kazi kwa Sifa"-Roma
"Wanauliza Roma siku hizi huimbi za kiharakati huku wakisema Ununio ndio kumbukumbu iliyobaki. Aaaaah.
Eeh kwani hutaki
Mbona hamkumsapoti Mange na ninyi mtakuwa wanafiki, Sijui mlikwama wapi.
Walinivunja dole la Mwisho waliacha Dole la kati. Eeh hii si ni nchi ya Democracy mkimaindi basi mnawajua sasa mbona hamuwakamati. Tuache hayo.
Vipi Korosho za Mtwara, Maana wapiga kura wengi ni Wakulima na Wafanya biashara.
Kumnyima mpinzani Ajenda, mtendee tu yaliyo mema.
Sio kumpelekea Difenda, mtaani tutie vilema.
Machozi ya Watanganyika hayatowaacha salama. Damu zilizomwagika milele zitawaandama.
Mwanangu akiwauliza wale walioniteka ni nani aliwatuma, MJIBUNI NIMEMZAA MPARE ILA SIMCHUKII MSUKUMA.
Nchi inaangamia viongozi hawana maarifa na hawataki wakosolewe wanafanya kazi kwa sifa"-Roma Zimbabwe #AnaitwaRoma. #Raupdates
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment