Ombi hilo limetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Hamadi Rashid Mohamed huko Ofisini kwake wakati akizungumza na Mwakilishi mkazi wa Shirika hilo kanda ya Zanzibar Maha Damaj, amesema Zanzibar imekuwa na uzalishaji mkubwa wa chakula, matunda na mboga mboga lakini bado kumekuwa na ongezeko la tatizo hilo nchini.
Alisema tatizo la utapiamlo huwaathari watoto wengi kutokana na kukosa vyakula vyenye afya ambalo limeonekana katika vituo vya afya na skuli.
Alisema ipo haja ya kufanya utafiti ili kujua njia ya kuondosha tatizo hilo pamoja na kuelimisha jamii juu ya madhara na kuwakinga watoto na madhara hayo.
“Watoto ndio taifa la kesho hivyo ipo haja yakuona wanakuwa vizuri kwa kupata vijana wenye afya na kulitumikia taifa lao badae”, alieleza Waziri Hamad.
Waziri Hamad alisema maeneo yaliyoathirika zaidi na tatizo hilo ni Wilaya Micheweni kwa upnde wa Pemba na Mkoa wa Kaskazini Unguja ni maeneo ambayo yameonekana kutokea kwa vifo vingi vya kinamama na watoto.
Nae Mwakilishi Mkazi Bi Maha Damaj Shirika lake litalishughulikia suala na kufanya utafiti na kuhakikisha kwamba wanalipatia ufumbuzi na kujua sababu ya tatizo hilo katika maeneo hayo.
Aidha alisema kuwa yupo tayari kuitangaza Zanzibar na kuifanya kuwa ni kituo cha elimu ya malaria kutokana na mafanikio makubwa ya kutokomeza maradhi hayo kwa asilimia 0.2 jambo ambalo ni faraja kubwa duniani.
Hata hivyo Muwakilishi huyo alisema kuwa shirika lake litatoa vifaa vya kina mama na watoto katika vituo vya afya 36 vya Unguja na Pemba.
No comments :
Post a Comment