Rais wa Zambia apiga panga mishahara ya wafanyakazi wa umma
Rais wa Zambia Edgar Lungu, hapo jana alitangaza kupunguzwa kwa mishahara ya wafanyikazi wa umma wanaolipwa mishahara ya juu kufuatia kuongezeka kwa bei ya mafuta na umeme.
Hatua hiyo inalenga kupunguza pigo kubwa kwa raia walio katika mazingira magumu, pia kupunguza kwa gharama ya safari za maafisa wakuu.
Mishahara hiyo itakatwa kati ya asilimia 15 na 20 na itaendelezwa hadi kwa wakurugenzi wa biashara zinazomilikiwa na serikali.
No comments :
Post a Comment